Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 10:14

Mafuriko Mauritius yamesababisha magari kuzama na uharibifu mwingine


Mafuriko yanayoendelea huko Mauritius na kupelekea uharibifu wa mali. January 15, 2024.
Mafuriko yanayoendelea huko Mauritius na kupelekea uharibifu wa mali. January 15, 2024.

Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mauritius ulitangaza utafungwa kuanzia saa kumi na nusu jioni kwa saa za huko hadi itakapotolewa taarifa zaidi

Mafuriko makubwa yaliikumba Mauritius siku ya Jumatatu wakati kimbunga cha hatari cha kitropiki kilipokuwa kinakaribia katika taifa hilo la kisiwa cha Bahari ya Hindi baada ya kukumba eneo la Reunion la Ufaransa.

Picha zilizochapishwa na vyombo vya habari vya eneo hilo katika kisiwa kidogo cha Paradise zilionyesha magari yakizama au kuchukuliwa na maji yaliyofurika mitaani. Uwanja wa ndege wa kimataifa ulitangaza kuwa utafungwa kuanzia saa kumi na nusu jioni kwa saa za huko hadi itakapotolewa taarifa zaidi wakati mabenki, ofisi za serikali na biashara nyingine za binafsi zikifunga ofisi na kuwarudisha wafanyakazi majumbani.

Idara ya Hali ya Hewa ya Mauritius (MMS) imesema katika taarifa yake kwamba tahadhari ya kimbunga cha daraja la tatu, kati ya viwango vinne imeanza kutumika na kuwashauri wananchi kukaa katika sehemu salama, huku hali ya mvua ikitarajiwa katika saa zijazo.

Forum

XS
SM
MD
LG