Maandamano dhidi ya vita vya Israel huko Gaza yamekuwa yakivutia maelfu ya watu nchini Morocco, tangu kuanza kwa ghasia hizo zaidi ya miezi miwili iliyopita, mengi yakiongozwa na makundi ya Kiarabu na Kiislamu.
Maandamano ya Jumapili yamepangwa kwa ushirikiano na makundi yenye msimamo wa mrengo wa kushoto na kundi lilipigwa marufuku lakini linastahmiliwa la Adl wal Ihasan Islamists.
Wengi wa waandamanaji hao takriban 10,000 walikuwa Waislamu, wanaume walikuwa kando na wanawake, wakati wakipeperusha vibendera vya Palestina, huku baadhi wakibeba mabango yenye maneno, “upinzani hadi ushindi,” “ sitisha uhusiano wa kawaida wa serikali ya Morocco na Israel” na “ uhuru wa Palestine.”
Morocco ilikubali kuimarisha uhusiano na Israel mwaka 2020, chini ya makubaliano yaliyosimamiwa na utawala wa Marekani na rais wa wakati huo Donald Trump ambaye pia aliijumuisha kutambua utawala wa Morocco juu ya eneo linalozozaniwa na Sahara Magharibi.
Waandamaji siku ya JUmapili pia walitaka kususiwa kwa bidhaa ambazo wanazishutumu zinaiunga mkono Israel.
Iasrael imeapa kuitokomeza Hamas, ambayo imetawala Gaza tangi mwaka 2007, baada ya wanamgambo wa Hamas kuvuka uzio wa mpakani hapo Oktoba 7 na kufanya mashambulizi dhidi ya miji ya Israel, ana kuua watu 1,200 na kuwashikilia mateka watu 240.
Forum