Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 07:45

Maelfu wajiunga na maandamano Hong Kong

Waandamanaji katika wilaya ya Mongkok, Hong Kong, Sept. 29, 2014.
Waandamanaji katika wilaya ya Mongkok, Hong Kong, Sept. 29, 2014.

Haya ni maandamano yenye ghasia zaidi huko Hong Kong tangu Beijing ilipochukua udhibiti wa eneo hilo lililokuwa zamani koloni ya Uingereza mwaka wa 1997.

Maelfu ya wanaharakati wa kidemokrasia waliandamana huko Hong Kong wakipuuza agizo la serikali kuondoka mitaani katika eneo hilo linalodhibitiwa na China, huku Beijing ikionya juu ya uingiliaji kati wa kigeni.

Polisi wafyatua gesi ya kutoa machozi dhidi ya waandamanaji katika wilaya yenye shughuli nyingi za kifedha mjini humo kabla ya kuondoka mwendo wa sita sita mchana, wakisema maandamano yanapungua. Lakini idadi ya waandamanaji iliongezeka majira ya jioni wakati watu wengi walikuwa wanaondoka kazini.

Haya ni maandamano yenye ghasia zaidi huko Hong Kong tangu Beijing ilipochukua udhibiti wa eneo hilo lililokuwa zamani koloni ya Uingereza mwaka wa 1997.

Uingereza imeomba kuwe na majadiliano yenye maana yatakayounga mkono demokrasia.

XS
SM
MD
LG