Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 00:06

Maelfu wajitokeza siku ya mwisho kumuaga Mandela


Kundi la waombolezaji wakishikilia picha ya Mandela huko Johannesburg, Afrika kusini
Kundi la waombolezaji wakishikilia picha ya Mandela huko Johannesburg, Afrika kusini
Kiasi cha waombolezaji 100,000 walijitokeza Ijumaa kuuaga mwili wa Rais wa zamani wa Afrika kusini, Nelson Mandela, ambao umewekwa kwenye jengo la serikali huko Pretoria kwa siku ya tatu na ya mwisho ya kuaga mwili huo.

Polisi walikuwa na kazi ngumu ya kudhibiti umati wa watu unaosubiri dakika za mwisho kutoa heshima zao kwa bwana Mandela kabla hajazikwa kijijini kwake, Qunu siku ya jumapili.

Mwandishi wa habari wa Sauti ya Amerika-VOA anasema baadhi ya waombolezaji walijaribu kuwasukuma polisi na vizuizi vya polisi. Anasema baadhi walishikwa na hasira wakati walipofahamu kuwa huwenda wasiweze kuuona mwili wa kiongozi huyo kabla ya saa ya mwisho kufika.

Watu kadhaa walianguka chini katika mkanyagano mdogo wakati waombolezaji walipoharakisha kupanda mabasi ambayo yaliwachukua kuelekea eneo la kuuga mwili. Waombolezaji walianza kupanga mistari tangu saa tisa alfajiri ya Ijumaa kwa saa za Afrika kusini.
XS
SM
MD
LG