Kwa upande wa Asia wa Istanbul, mkutano wa hadhara wa Kadikoy ulishuhudia washiriki wa vikundi kadhaa vya wanawake wakisikiliza hotuba, kwa kucheza na kuimba.
Maandamano hayo ya kupendeza yalisimamiwa na polisi wengi, wakiwemo askari waliovalia mavazi ya kuzuia ghasia na lori la maji ya kuwasha.
Serikali ya Rais Recep Tayyip Erdogan, ilitangaza 2025 kuwa Mwaka wa Familia. Waandamanaji walipinga wazo la kuamini jukumu la wanawake ni kuwa wake na wazazi tu, wakiwa wamebeba mabango yenye maandishi “Familia haitatufunga kimaisha” na “Hatutatolewa kwa ajili ya familia tu.”
Wakosoaji wameishutumu serikali kwa kusimamia vikwazo vya haki dhidi ya wanawake na kutofanya vya kutosha kukabiliana na unyanyasaji wa wanawake.
Forum