Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 16, 2025 Local time: 18:11

Maduro atakutana na kiongozi mwenzake wa Guyana huku mivutano ikiongezeka


Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro akiwa Caracas. November 20, 2023.
Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro akiwa Caracas. November 20, 2023.

Mkutano huo ambao umepangwa kufanyika katika kisiwa cha Caribbean cha St. Vincent ulitangazwa kufuatia mazungumzo ya Maduro na Waziri Mkuu wa St. Vincent na Grenadines, na rais wa jumuiya ya Latin Amerika na mataifa ya Caribbean (CELAC), Ralph Gonsalves pamoja na Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro atakutana Alhamisi na mwenzake wa Guyana, Mohamed Irfaan Ali, huku mivutano ikiongezeka juu ya mamlaka ya eneo lenye utajiri wa mafuta la Essequibo.

Mkutano huo ambao umepangwa kufanyika katika kisiwa cha Caribbean cha St. Vincent, ulitangazwa kufuatia mazungumzo ya Maduro na waziri mkuu wa St. Vincent na Grenadines, na rais wa jumuiya ya Latin Amerika na mataifa ya Caribbean (CELAC), Ralph Gonsalves, pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres siku ya Jumamosi.

Rais wa Guyana Mohamed Irfaan Ali katika picha iliyochukuliwa May 30, 2023.
Rais wa Guyana Mohamed Irfaan Ali katika picha iliyochukuliwa May 30, 2023.

Ali, ambaye alikubali mkutano huo licha ya bunge lake kwa kauli moja kumwambia asiende, alisema kuwa mpaka wa ardhi wa Guyana hautakuwepo katika majadiliano.

Migogoro juu ya mkoa wa Essequibo ni ya muda mrefu, ingawa ugunduzi wa hivi karibuni wa mafuta na gesi kwenye ufukwe umesababisha mivutano juu ya suala hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG