Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 01, 2022 Local time: 10:22

Macron asema haki za binadamu sio sharti la uuzaji Silaha kwa Misri


Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron,kulia alipokutana na rais wa Misri Abdel-Fattah el-Sissi huko katika jumba la Elysee mjini Paris.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema Jumatatu kwamba hatatoa masharti katika uuzaji wa silaha kwa Misri juu ya haki za binadamu kwa sababu hakutaka kudhoofisha uwezo wa Cairo wa kukabiliana na ugaidi katika eneo hilo, maoni ambayo yanaweza kukasirisha wakosoaji.

Rais huyo alipinga ukosiaji katika uhusiano wake wa karibu na rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi, akisema kwamba kuchukua hatua kali juu ya kuheshimu haki za binadamu itakuwa hakuna tija. Macron alimkaribisha Sisi, ambaye alimtaja kama rafiki yake kwa mazungumzo katika siku ya pili ya ziara ya serikali ya Misri ya siku tatu nchini Ufaransa.

Kabla ya majadiliano yao Amnesty International na vikundi vingine vya haki vya haki za binadamu viliituhumu Ufaransa kwa kuvumilia kwa muda mrefu ukandamizaji wa Rais al-Sisi wa aina yoyote ya upinzani na kusema sasa muda kwa Macron kutetea haki za binadamu.

Lakini kiongozi huyo wa Ufaransa aliepuka kumkosoa moja kwa moja aliyekuwa jenerali wa jeshi al-Sisi, ambaye amewashambulia wafuasi wa rais aliyeondolewa madarakani Mohammed Morsi, na vile vile kwa wale wenye mrengo wa kushoto na waliberali.

Uhusiano wa kimkakati na haki za binadamu

Macron aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano wa Pamoja akiwa na Sisi kwamba alikuwa amezungumzia suala la haki za binadamu wakati wa majadiliano yao na akasema amebaki kuwa mtetezi wa mara kwa mara wa uwazi wa kidemokrasia na kijamii.

“Sitaweka masharti juu ya masuala ya ulinzi na ushirikiano wa kiuchumi juu ya kutokubaliana (juu ya haki za binadamu), kwanza kwa sababu ninaamini juu ya uhuru wa watu na kwa heshima ya masilahi yetu halali na ya pande mbili. Pia, nadhani ni bora kuwa na sera ya kudai mazungumzo kuliko kususia ambayo itapunguza tu ufanisi wa washirika wetu katika mapambano dhidi ya ugaidi na kwa hali ya utulivu wa kikanda.” alisema Macron.

Nchi zote mbili ambazo zina wasiwasi juu ya kukosekana kwa utulivu kote Sahel, vitisho kutoka kwa vikundi vya jihadi huko Misri na ombwe la kisiasa nchini Libya, zimekuza uhusiano wa karibu wa kiuchumi na kijeshi wakati Rais al-Sisi anashamiri madarakani.

Macron na al-Sisi pia wana wasiwasi kuhusu tuhuma za Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, ambaye aliongoza wito wa maandamano dhidi ya Ufaransa na migomo mnamo mwezi Oktoba juu ya utetezi wa Macron wa haki ya kuchapisha katuni zinazomdhihaki Mtume Muhammad.

Macron alizungumzia juu ya katuni wakati wa kumbu kumbu ya mwalimu wa shule Samuel Paty ambaye alikatwa kichwa na mtu mwenye msimamo mkali wa Kiisilamu mwezi Oktoba kwa kuwaonyesha wanafunzi wake katuni za Mtume Muhammad darasani wakati wa darasa la uhuru wa kujieleza.

“Ni muhimu sana kwamba wakati tunatoa maoni yetu, kwamba hatufanyi kwa sababu ya maadili ya kibinadamu, tukiuke maadili ya kidini. Kiwango cha maadili ya kidini ni cha juu sana kuliko maadili ya wanadamu.” alisema Al -Sissi.

Kiongozi huyo aliongeza kusema kuwa maadili ya kibinadamu yameundwa na yanaweza kubadilishwa wakati wowote, lakini maadili ya kidini ni matakatifu kuliko kila kitu. Viongozi hao wawili pia walizungumza kwa kirefu juu hali inayoboreka nchini Libya na mvutano unaoongezeka kati ya Ufaransa na Uturuki na hali ya mashariki ya kati kwa ujumla.

Imetayarishwa na Sunday Shomari, VOA Washington DC

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG