Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 21:58

Macron aitembelea Israel kuonyesha mshikamano, ahimiza ulinzi wa Wapalestina huko Gaza


Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akimsalimia Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron baada ya mkutano wao wa pamoja na waandishi wa habari, Oktoba 24, 2023.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akimsalimia Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron baada ya mkutano wao wa pamoja na waandishi wa habari, Oktoba 24, 2023.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron Jumanne ameitembelea Israel akipeleka ujumbe wa mshikamano na Israel kufuatia shambulio baya la Hamas lakini pia akishinikiza ulinzi wa raia wa Palestina huko Ukanda wa Gaza.

Macron amemwambia Rais wa Israel Isaac Herzog kwamba kilichotokea “haikotosahaulika kamwe” na kwamba kipaumbele cha kwanza ni kuachiliwa huru mateka wote wanaoshikiliwa na Hamas.

“Nataka muelewe kwamba hamko peke yenu katika vita hivi dhidi ya ugaidi,” Macron amesema.

Jeshi la Israel leo limesema liliendesha mashambulizi ya anga huko Gaza, ikiwemo kulenga makao makuu ya operesheni za Hamas na kuua manaibu kamanda kadhaa wa kundi hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG