Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 14:53

Macron ayaomba mataifa ya Asia Pacific yaishinikize Russia kuacha mapigano


Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akiwa akiwa kwenye mkutano wa APEC nchini Thailand. Nov. 18, 2022.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akiwa akiwa kwenye mkutano wa APEC nchini Thailand. Nov. 18, 2022.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron Ijumaa ametoa wito kwa viongozi kuiomba Russia ikomeshe vita vyake nchini Ukraine.

Macron amesema hayo wakati wa hotuba yake mbele ya kongamano la ushirika wa mataifa ya Asia Pacific, APEC mjini Bangkok Thailand. Amesema kwamba kando na Ufaransa kuwa kwenye mstari wa mbele kuisaidia Ukraine, pia inatazamia kushirikiana na mataifa mengine kama vile China , India pamoja na eneo la Mashariki kwa ujumla.

Kando na mataifa hayo amesema ni muhimu kuwa na juhudi za kila mmoja katika kushinikiza kukomeshwa kwa mapigano hayo. Mkutano wa APEC unalenga kuimarisha masuala ya kiuchumi ya kieneo kwa kuweka mikakati ya muda mrefu ya soko huru.

XS
SM
MD
LG