Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 22:58

Machar amemteuwa Paulino kuwakilisha Sudan Kusini katika UN


Kiongozi wa waasi Sudan Kusini, Riek Machar.
Kiongozi wa waasi Sudan Kusini, Riek Machar.

Kiongozi wa waasi huko Sudan Kusini, Riek Machar amemteuwa mwakilishi mpya kwenye Umoja wa Mataifa akipendekeza kwamba mwakilishi wa awali, Miyong Kuon huwenda akabadili mtazamo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Asociatted Press-AP, Machar amekuwa akishuhudia wimbi la kuangushwa madarakani kutoka upande wake na kupelekea mashindano kwa baadhi ya wafuasi wake na wale wa mtangulizi wake Deng Gai ambaye anajiita kiongozi wa kundi.

Kwa mujibu wa nakala ya Januari tisa mwaka huu wa 2017, Machar alimteuwa Ukuni Michael Paulino kama mwakilishi mpya kwenye Umoja wa mataifa. Ofisa huyo mpya atatakiwa kukaa makao makuu ya Umoja wa Mataifa ili kufuatilia maendeleo yanayofanyika juu ya nchi hiyo.

XS
SM
MD
LG