Mamia ya waandamanaji walijaribu kulivamia eneo la Green Zone lenye ulinzi mkali mjini Baghdad ambalo lina ofisi za balozi za kigeni na makao makuu ya serikali ya Iraq mapema Jumamosi kufuatia ripoti kwamba kundi moja la kizalendo lilichoma nakala ya kuruan mbele ya ubalozi wa Iraq mjini Copenhagen.
Vikosi vya usalama viliwarudisha nyuma waandamanaji ambao walifunga daraja la Jumhuriya linaloelekea Green Zone, na kuwazuia waandamanaji hao kufika ubalozi wa Sweden.
Maandamano yamekuja siku mbili baada ya watu kukasirishwa na mpango ulioandaliwa wa kuchoma kitabu kitakatifu cha ki-islam huko Sweden, walishambulia ubalozi wa Sweden mjini Baghdad. Waandamanaji walizingira jengo la kidiplomasia kwa saa kadhaa, wakipeperusha bendera na mabango yanayowaonyesha wafuasi wa wanachama wa kishia nchini Iraq na kiongozi wa kisiasa Muqtada al-Sadr na kuwasha moto.
Wafanyakazi wa ubalozi waliondolewa siku moja kabla. Saa kadhaa baadae Waziri Mkuu wa Iraq alisitisha ushirikiano wa kidiplomasia na Sweden kufuatia maandamano ya kuidhihaki Quran.
Forum