Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 16, 2025 Local time: 18:46

Maandamano yamevuruga hali nchini Georgia


Waandamanaji waliorushia polisi vilipuzi Nov 30 2024
Waandamanaji waliorushia polisi vilipuzi Nov 30 2024

Watu 107 wamekamatwa nchini Georgia leo Jumamosi katika siku ya pili ya maandamano ya kupinga uamuzi wa serikali kuchelewesha mazungumzo kuhusu mapendekezo ya nchi hiyo kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Maandamano yanafanyika wakati kuna mgogoro mkubwa wa baada ya uchaguzi mkuu.

Georgia imekumbwa na vurugu tangu chama cha Georgian Dream kudai kushinda uchaguzi wa bunge uliofanyika Oktoba 26.

Wanasiasa wa upinzani, wanaopendelea nchi hiyo kujiunga na Umoja wa Ulaya, wamedai kwamba uchaguzi ulikumbwa na udanganyifu.

Wizara ya Mambo ya Ndani imesema watu 107 wamekamatwa kwa kutotii amri za polisi na kushiriki katika visa vya ghasia.

Wizara hiyo imesema kwamba maandamano yamefanyika usiku mzima, waandamanaji wakiwarushia maafisa wa usalama mawe, vyuma na vitu vingine na kwamba wafanyakazi wa wizara ya mambo ya ndani wamejeruhiwa. Polisi 32 wamejeruhiwa.

Waziri Mkuu Irakli Kobakhidze alisema Alhamisi kwamba Georgia haitaanzisha mazungumzo ya kutaka kujiunga na Umoja wa Ulaya hadi mwaka 2028, matamshi ambayo yamepelekea maandamano ya siku mbili.

Forum

XS
SM
MD
LG