Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 14:21

Maandamano yaendelea Misri


waandamanaji mjini Cairo

Mamia ya waandamanaji wavuruga uchukuzi mjini Cairo

Mamia ya wanaharakati wanaopigania mabadiliko ya kiutawala nchini Misri wamevuruga shughuli za uchukuzi katikati ya mji mkuu wa Cairo Jumapili na kuweka vizuizi kuelekea jengo kuu la serikali katika siku ya tatu ya maandamano kupinga utawala wa kijeshi nchini humo. Baada ya kulala kwa siku ya pili katika kambi ya kuezekwa kwenye uwanja wa Tahrir Square mjini Cairo,wanaharakati hao waliziba barabara na kulizingira jengo la utawala la Mogamma Jumapili.Wanaharakati hao walianza maandamano Ijumaa kama sehemu ya upinzani mkubwa kote nchini misri, wakidai hatua za haraka za kuwashitaki maafisa wa ulinzi wanaolaumiwa kwa mauaji ya waandamanaji wakati wa upinzani mkali na maandamano yaliyoanza mwezi Februari na kumng’oa madarakani rais Hosni Mubarak. Waandamanaji pia wanataka utawala wa kijeshi ukomeshe kabisa kuwashitaki raia katika mahakama za kijeshi na waharakishe kesi dhidi ya maafisa wa enzi ya Mubarak walioshtakiwa kwa ufisadi.

XS
SM
MD
LG