Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 23:57

Maandamano ya Upinzani yatawanya wa polisi DRC.


Polisi wa kukabiliana na ghasia wakitawanya waandamanaji wa upinzani mjini Kinshasa. Desemba 27, 2023.
Polisi wa kukabiliana na ghasia wakitawanya waandamanaji wa upinzani mjini Kinshasa. Desemba 27, 2023.

Polisi nchini Congo Jumatano wametumia gesi ya kutoa machozi kutawanya maandamano yaliyoitishwa na upinzani katika mji mkuu wa Kinshasa, wakitaka kurudiwa kwa uchaguzi wa rais na bunge uliofanyika wiki iliyopita na kuzua taharuki.

Uchaguzi huo wenye utata unatishia kuliyumbisha taifa hilo maskini ambalo tayari linakabiliana na tatizo la usalama upande wa mashariki, hali inayodumaza maendeleo, wakati likiongoza ulimwenguni kwa uzalishaji wa madini ya cobalt miongoni mwa mengine muhimu.

Wagombea watano wa urais, wapinzani wa rais Felix Tshisekedi kwenye uchaguzi huo waliwaomba wafuasi wao kushiriki kwenye maandamano ya Jumatano, ili kupinga zoezi hilo wanalodai lilikumbwa na udanganyifu, na kwa hivyo libatilishwe.

Waliapa kuendelea na maandamano hayo hata baada ya serikali kuyapiga marufuku Jumanne, ikisema kwamba yanahujumu kazi ya tume ya taifa ya uchaguzi, CENI, wakati ikiendelea na zoezi la kukusanya matokeo, ambapo kwa sasa yanaonyesha kuwa Tshisekedi anaongoza kwa kura nyingi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, polisi walizingira makao makuu ya mgombea mmoja wa upinzani, Martin Fayulu, ambako waandamanaji walitarajiwa kukusanyika.

Forum

XS
SM
MD
LG