Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 05, 2024 Local time: 15:20

Maandamano ya upinzani Congo yasababisha vifo


Waandamanaji wa upinzani mjini Kinshasa, DRC, Sept. 19, 2016.
Waandamanaji wa upinzani mjini Kinshasa, DRC, Sept. 19, 2016.

Zaidi ya watu 44 wameuwawa nchini Congo katika muda wa siku mbili za mapambano ya mtaani kati ya vikosi vya usalama na waandamanaji wenye hasira kufuatia kucheleweshwa kwa uchaguzi wa urais, mtafiti mwandamizi wa kundi la haki za binadamu la Human Rights Watch alisema Jumanne.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press-AP polisi walisema zaidi ya watu 100 wamekamatwa katika ghasia hizo. Maelfu ya watu waliingia mitaani katika mji mkuu wa Congo, Kinshasa, siku ya Jumatatu kupinga kucheleweshwa kwa uchaguzi wa urais ambapo wanasema ni juhudi za Rais Joseph Kabila za kutaka kuendelea kuwepo madarakani baada ya muda wake wa uongozi kuisha mwishoni mwa mwezi Disemba.

Maandamano ya upinzani nchini DRC
Maandamano ya upinzani nchini DRC

Mahakama kuu ilisema Kabila anaweza kuendelea kuwepo madarakani hadi hapo kiongozi mpya atakapochaguliwa. Tume ya uchaguzi nchini humo imeeleza sababu za kuchelewa kwa uchaguzi ambao ulipangwa kufanyika mwezi Novemba ikisema orodha ya uandikishaji wapiga kura haitakuwa tayari.

Milio ya risasi ilisikika Jumanne mjini Kinshasa huku mivutano ikiongezeka na magari yakichomwa moto na takribani mitaa yote ikiwa haina watu.

XS
SM
MD
LG