Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 17:16

Wafuasi wa muungano wa CORD Kenya wakiuka amri ya serikali


Wafuasi wa muungano wa CORD nchini Kenya wakikimbia baada ya polisi wa kutuliza ghasia mjini Nairobi, Julai 7, 2014.
Wafuasi wa muungano wa CORD nchini Kenya wakikimbia baada ya polisi wa kutuliza ghasia mjini Nairobi, Julai 7, 2014.

Wafuasi wa muungano wa kisiasa nchini Kenya, CORD, wamekiuka amri ya Serikali kutofanya maandamano mjini Nairobi na badala yake wakajitokeza kwa wingi kuishinikiza Tume ya Uchaguzi na mipaka nchini humo, IEBC, ing’atuke afisini.

Gazeti la Daily Nation limeripoti kwamba wafuasi wa upinzani walianza kukusanyika nje ya jengo la Anniversary Towers, ambalo ndilo makao makuu ya tume hiyo, kuanzia saa moja asubuhi, licha ya kuwepo maafisa wengi wa usalama waliokuwa wakilinda doria.

Vinara wa Muungano huo, Raila Odinga, Kalonzo Musyoka na Moses Wetanguala, waliwahutubia wafuasi wao, huku Kalonzo akisema kwa sauti kuu, IEBC ni lazima iondoke afisini na kwamba hakuna haja ya polisi kurusha gesi ya kutoa machozi kwa waandamanaji kwani maandamano yao ni ya amani. Mjini Kisumu, mamia ya watu walionekana kukusanyika nje ya afisi za tume hiyo.

Hii ni mara ya pili kwa muungano huo wa Cord kuitisha maandamano huku viongozi wake wakisema hawatashiriki kwenye uchaguzi wa mwaka ujao iwapo makamishina wa tume hiyo hawataondolewa na kubadilishwa na wale ambao wanakubalika na pande zote mbili.

Waziri wa mambo ya ndani, Joseph Nkaissery, ameonya kwamba visa vyovyote vya uvunjaji wa sheria wakati wa maandamano hayo, vitakabilianwa navyo vikali na polisi.

XS
SM
MD
LG