Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 23:39

Maandamano mapya yazuka Syria


waandamanaji wa syria
waandamanaji wa syria

Maandamano mapya yamezuka kote Syria ijumaa siku moja baada ya Serikali kutangaza hatua za mageuzi yenye lengo la kukidhi matakwa ya waandamanaji.

Maandamano mapya yamezuka kote Syria ijumaa siku moja baada ya Serikali kutangaza hatua za mageuzi yenye lengo la kukidhi matakwa ya waandamanaji.

Maandamano ya kupinga utawala wa chama cha Baath yalifanyika baada ya sala ya ijuma katika miji mitatu ya Syria ikiwemo mji mkuu, Damascus.

Shirika la habari la associated press liliripoti kuwa takriban watu elfu tano wanaodai uhuru zaidi walikusanyika katika mji wa Daraa kitovu cha maandamano ya hivi karibuni.

Mikutano ya upinzani imekuwa ni kitisho kikubwa kuwahi kukabili utawala wa miaka 11 ya rais wa Syria Basher Al Assad na mamlaka ya muda mrefu ya familia yake.

Hatua za mageuzi ya Serikali zilitangazwa na bwana Asaad alhamisi ikiwemo kuunda tume ya kutafiti uwezekano wa kuondoa sheria ya dharura nchini humo.

XS
SM
MD
LG