Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 23:39

Maandamano makubwa ya kupinga hali nchini Ethiopia yafanyika Marekani


Mamia ya watu waandamana mjini Washington DC kupinga hali inayoendelea nchini Ethiopia.
Mamia ya watu waandamana mjini Washington DC kupinga hali inayoendelea nchini Ethiopia.

Mamia ya watu walijiunga katika maandamanano ya amani Alhamisi yaliyoandaliwa na watu wa Tigray wanaoishi au kufanya kazi katika mji mkuu wa  Marekani, Washington DC, na maeneo jirani, kupinga hali inayoendelea nchini Ethiopia.

Hayo yalijiri wakati wa maadhimisho ya mwaka mmoja wa mzozo wa jeshi la serikali pamoja na vikosi vya wapiganaji kutoka mkoa wa kaskazini wa Tigray.

Waandamanaji walitembea kutoka eneo la bunge hadi kwenye ofisi za kimataifa za maendeleo mpaka wizara ya mambo ya nje ya marekani.

“Tunazunguuka katika eneo hili kimsingi tukihamasisha juu ya kile ambacho kimekuwa kikifanyika huko Tigray sehemu ya kaskazini zaidi ya Ethiopia kwa mwaka jana. kwa sasa Tigray imezingirwa , kuna kukatika kwa umeme , kukatika kwa mawasiliano, kuna ubakaji wa kutumia silaha, na njaa ya kutumia silaha hicho ndio kinatokea sasa," alisema mmoja wa waandamanaji.

Waandamanaji mjini Washington DC Nov. 4, 2021. (Sara Fissehaye, VOA)
Waandamanaji mjini Washington DC Nov. 4, 2021. (Sara Fissehaye, VOA)

Waandamanaji waliimba nyimbo huku wakibeba mabango yaliyoshutumu serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed kwa "kufanya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Tigray na kuwatumbukiza katika njaa."

“Niko hapa kuwa sauti ya watu wangu, na tuko hapa kuandaa maandamano haya hasa kwa ajili ya marekani, Umoja wa Mataifa wahitaji kuchukua hatua. Wamekuwa wakisema tu lakini kusema hakutopshi."

Waandamanaji wengi walibeba bendera za rangi nyekundu na dhahabu za mkoa wa Tigray. Wengine walijiunga katika maandamano hayo wakitokea majimbo ya mbali kama vile California na Washington.

XS
SM
MD
LG