Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 06, 2023 Local time: 22:56

Maandamano makali yashuhudiwa Armenia


Picha ya zamani ya maandamano Armenia

Maelfu ya waandamanaji Jumanne wamekusanyika kwenye mji mkuu wa Armenia wa Yerevan, wakiongozwa na upinzani kwenye kampeni ya kushinikiza waziri mkuu Nikol Pashinyan, ajiuzulu kutokana na mkataba wa mwezi Novemba na Azerbaijan ikilenga kusitisha mapigano.

Waandamanaji hao waliokuwa kwenye bustani kuu mjini humo walisikika wakisema kuwa Nikol ni msaliti wakati maafisa wa usalama wakishika doria kwenye ofisi za kiongozi huyo zilizoko karibu.

Kundi lingine linasemekana kuingia kwenye majengo ya serikali na kuzua vurugu huku wengine wakisemekena kufunga barabara kuu. Kiongozi wa muungano wa upinzani wenye vyama zaidi ya darzeni moja ameapa kuitisha maandamano ya kila siku hadi pale Pashinyan atakapo kubali kukabidhi madaraka kwa serikali ya mpito itakayo twikwa jukumu la kuitisha uchaguzi wa bunge ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.

Vazgen Manukian ambaye ameidhinishwa na muungano huo kwa jina National Salvation Movement, kuongoza serikali ya mpito ameomba jeshi la Armenia pamoja na polisi kukaidi amri za Pashinyan na kujiunga na watu wengine. Awali Pashinyan aliweka wazi kuwa hakuwa na nia ya kuondoka madarakani.

Imetayarishwa na Harrison Kamau

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG