Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:01

Maandamano yaendelea Malawi


Polisi wa kupambana na ghasia wakifanya doria mjini Lilongwe, Malawi
Polisi wa kupambana na ghasia wakifanya doria mjini Lilongwe, Malawi

Waandamanaji wapinga utawala wa rais Bingu wa Mutharika

Rais wa Malawi Bingu wa Mutharika ametoa mwito wa utulivu baada ya watu wanane kupigwa risasi na kuuawa na polisi wakiandamana kupinga serikali yake. Rais Mutharika alihutubia taifa kupitia radio Alhamis akisema yupo tayari kukaa chini na kuzungumza na wapinzani wake. Maandamano makali yalizuka Jumatano wiki hii katika miji mitatu mikubwa nchini humo, Blantyre, Mzuzu na mji mkuu Lilongwe. Maafisa wanasema waliouawa walipigwa risasi na polisi katika mji wa Mzuzu. Mashahidi wanasema waandamanaji pia walipora maduka na kuwasha mioto huku polisi wakijibu kwa kufyatua gesi ya kutoa machozi. Waandamanaji wanasema wamechoshwa na uhaba wa mafuta ya petroli, ongezeko la bei za bidhaa na kunyimwa uhuru wao wa kimsingi. Lakini watu waliozungumza na sauti ya Amerika wanasema idadi ya waandamanji waliouawa kufikia Alhamis, imeongezeka.

XS
SM
MD
LG