Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 17:41

Maafisa watano wa polisi watiwa kizuizini


Meya wa mji wa Baltimore, Stephanie Rawlings-Blake akizungumza juu ya kifo cha Freddie Gray kilichotokea mwezi uliopita
Meya wa mji wa Baltimore, Stephanie Rawlings-Blake akizungumza juu ya kifo cha Freddie Gray kilichotokea mwezi uliopita

Rais wa Marekani Barack Obama akiwa huko White House alisema Ijumaa kwamba ni muhimu kabisa kwamba ukweli unajitokeza juu ya kile kilichotokea kufuatia kifo cha Freddie Gray mkazi wa Baltimore, katika jimbo la Maryland aliyefariki mwezi uliopita akiwa mikononi mwa polisi.

Maafisa sita wa polisi katika mji wa Baltimore waliohusika katika kesi ya Freddie Gray walifunguliwa mashtaka mapema Ijumaa na mwendesha mashtaka mkuu wa mji wa Baltimore Marilyn Mosby. Mwendesha mashtaka huyo alitangaza kuna sababu ya msingi ya kufungua mashtaka ya uhalifu dhidi ya maafisa sita waliohusika katika kumkamata Freddie Gray akisema uchunguzi wa kitabibu katika kitengo cha serikali umegundua kwamba kifo chake kilichotokea mwezi uliopita akiwa mikononi mwa polisi ni mauaji.

Wakati huo huo, Meya wa mji wa Baltimore, Stephanie Rawlings-Blake alisema “alihudhunishwa na kusikitishwa” na mashtaka hayo. Alisema maafisa polisi watano kati ya sita waliohusika katika kumkamata Gray wapo kizuizini na kwamba alimuagiza kamishna wa polisi katika mji wa Baltimore kuwasimamisha kazi haraka kwa muda maafisa wote sita.

Meya Stephanie alisema “tunajua kwamba maafisa wengi katika idara ya polisi ya mji wa Baltimore wanahudumu mji wetu kwa hadhi, hamasa na heshima pamoja na tahadhima lakini kwa wale ambao wanataraji kujihusisha na mauaji, uonezi, ubaguzi na rushwa wacha niwe muwazi kwa hili ni kwamba hakuna nafasi kwa hilo katika idara ya polisi ya mji wa Baltimore,” alisema na kuahidi kwamba sheria itachukua mkondo wake.

Tangazo la Ijumaa la kufunguliwa mashtaka kwa maafisa wa polisi waliohusika na kifo cha Gray lilipokelewa kwa furaha ikizingatiwa hivi karibuni kumekuwepo na shutuma kwa jeshi la polisi juu ya namna linavyawatendea wanaume weusi pale wanapowakamata n a hata kusababisha kifo kwa baadhi yao jambo ambalo lilizusha maandamano nchi nzima na kutoa wito wa kuangaliwa sheria dhidi ya jeshi la polisi na wanaume weusi.

XS
SM
MD
LG