Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 20, 2024 Local time: 14:28

Maafisa wafika Dallas kwa uchunguzi wa ajali ya ndege


Mabaki ya ndege ambazo zimegongana angani katika uwanja wa ndege wa Dallas Executive Airport, Jumamosi, November 12, 2022.
Mabaki ya ndege ambazo zimegongana angani katika uwanja wa ndege wa Dallas Executive Airport, Jumamosi, November 12, 2022.

Maafisa wa idara ya Marekani ya usafirishaji wapo jijini Dallas, Texas kuchunguza sababu za ajali ya ndege mbili zilizo gongana hewani wakati wa maonyesho ya ndege na kuua watu sita.

Ndege za kivita za wakati wa vita vya pili vya dunia ziligongana na kuanguka baada ya kutokea mlipuko mkubwa siku ya Jumamosi katika uwanja wa ndege wa Dallas Executive uliopo kilometa 16 kutoka katikati ya jiji.

Ajali hiyo imetokea baada ya kupita miaka mitatu baada ya ndege ya kivita jimboni Connecticut kupata ajali na kuuwa watu saba, ikiwa bado kuna wasiwasi kuhusu usalama wa maonyesho ya ndege yanayo husisha ndege za zamani za kivita.

Kampuni ambayo inamiliki ndege hizo katika maonyesho ya ndege ya Wings Over Dallas imewahi kuwa na ajali nyingine katika historia yake ya miaka 60.

XS
SM
MD
LG