Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 28, 2025 Local time: 11:44

Maafisa wa ngazi za juu Sudan Kusini wametajwa kwa ukiukaji wa waki za binadamu


Yasmin Sooka, mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini
Yasmin Sooka, mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini

Viongozi wa juu wa serikali na jeshi walitajwa katika ripoti mpya ya Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini ambayo inaelezea jukumu la serikali kwa mauaji makubwa, ubakaji na utumwa wa ngono

Jopo la Umoja wa Mataifa la wataalamu wa haki za binadamu Jumatatu limewataja maafisa kadhaa wa ngazi ya juu wa Sudan Kusini wanasema kwamba wanastahili kuchunguzwa kwa uhalifu na kushtakiwa kwa kuhusika kwao katika ukatili mkubwa dhidi ya raia.

Viongozi wa juu wa serikali na jeshi walitajwa katika ripoti mpya ya Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini ambayo inaelezea jukumu la serikali kwa mauaji makubwa, ubakaji na utumwa wa ngono. Tume hiyo ambayo ilifanya uchunguzi wa mwaka mmoja katika majimbo sita nchini Sudan Kusini na kutoa sehemu ya matokeo yake mwezi Machi ilisema hakuna hata mmoja kati ya wale waliotajwa katika ripoti ya mwisho aliyekabiliwa na uwajibikaji wowote kwa uhalifu wao.

"Kwa miaka kadhaa, ugunduzi wetu umekuwa ukionyesha mara kwa mara kwamba kutokhofia kushtakiwa kwa uhalifu mkubwa ni kichocheo kikuu cha ghasia na taabu zinazowakabili raia nchini Sudan Kusini," mwenyekiti wa tume hiyo Yasmin Sooka alisema. "Kwa hivyo tumechukua hatua ya kuwataja zaidi watu wanaotakiwa kufanyiwa uchunguzi wa jinai na kushtakiwa kwa jukumu lao katika ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.

XS
SM
MD
LG