Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 16, 2025 Local time: 11:22

Maafisa wa Mexico walikata maji kwenda Mexico City na kusababisha uharibifu


Mfano wa mfumo wa mabomba ya usambazaji maji ambayo yalikatwa na maafisa wa Mexico.
Mfano wa mfumo wa mabomba ya usambazaji maji ambayo yalikatwa na maafisa wa Mexico.

Mvua isiyo ya kawaida ya kiwango kidogo imeharibu mfumo wa Cutzamala, mtandao wa mabwawa matatu yanayohudumia wakazi zaidi ya milioni 20 katika Bonde la Mexico kwa viwango vya chini katika historia ya msimu

Maafisa wa Mexico walikata usambazaji wa maji kwa mwezi mmoja kwenda Mexico City usiku wa manane Ijumaa na kulifanyia kazi suala hilo takribani mwezi mmoja baada ya masharti ya awali kuamriwa wakati ukame ukikausha hifadhi za mji mkuu.

Tume ya Taifa inayohusika na masuala ya Maji nchini Mexico na Meya wa Mexico City walitangaza hatua hiyo katika mkutano na waandishi wa habari lakini maafisa hawakuripoti kukatwa kwa maji kupitia mitandao ya kijamii hadi saa nne kabla ya zoezi kuanza kutekelezwa.

Mvua isiyo ya kawaida ya kiwango kidogo imeharibu mfumo wa Cutzamala, mtandao wa mabwawa matatu yanayohudumia wakazi zaidi ya milioni 20 katika Bonde la Mexico kwa viwango vya chini katika historia ya msimu. Mfumo huo ni asilimia 44 chini kuliko inavyopaswa kuwa wakati huu wa mwaka.

Maafisa walianza kuweka masharti kwenye maji kutoka Cutzamala kwa takriban asilimia 8 hapo Oktoba 17. Kukatika maji siku ya Ijumaa ni tatizo kubwa ambalo linawakilisha zaidi ya asilimia 25 ya mtiririko wa jumla katika mfumo. Maeneo 12 hasa magharibi mwa mji yanaweza kutarajia mtiririko wa kiwango cha chini cha maji hadi vizuizi viondolewe, maafisa walisema.

Forum

XS
SM
MD
LG