Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 16:29

Maafisa wa Marekani wazuia njama za Alqaeda


Rais wa Marekani Baracka Obama alipewa taarifa za njama hizo kwanza.
Rais wa Marekani Baracka Obama alipewa taarifa za njama hizo kwanza.

Rais wa Marekani Barack Obama alipewa taarifa kwanza kuhusu njama hizo.

Maafisa wa Marekani wanasema wamezuia njama za ulipuaji bomu za alqaeda zilizolenga kulipua ndege iliyokuwa ikisafiri kuja Marekani .

Maafisa hapa Marekani wanasema tawi la alqaeda huko Yemen lilidhamiria kumweka mlipua mabomu wa kujitoa muhanga kwenye ndege iliyokuwa ikielekea Marekani, milipuko ilikuwa imefungwa kwenye nguo za ndani za mlipuaji huyo.

Wanasema njama hizo ziligunduliwa na bomu hilo kukamatwa kabla ndege yeyote kuingia hatarini.

Baraza la taifa la usalama la White House limesema kwenye taarifa yake jumatatu kuwa rais wa Marekani Barack Obama alipewa taarifa kwanza kuhusu njama hizo mwezi Aprili na kupata taarifa za kila wakati kuhusu hali hiyo. Ilisema rais alihakikishiwa kwamba chombo hicho hakileti hatari kwa umma.

XS
SM
MD
LG