Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 14:22

Maafisa wa China watuhumiwa kununuwa pembe za ndovu Tanzania


Ndovu wa Afrika Mashariki
Ndovu wa Afrika Mashariki

Ununuzi wa pembe hizo ulifanya bei yake kupanda maradufu na kufikia dola za kimarekani 700 kwa kilo moja. Wanadiplomasia wa China, maafisa wa kijeshi na wafanya biashara wa China siku za nyuma walitumia ziara kama hizo kununua shehena kubwa ya pembe za ndovu Tanzania.

Ripoti mpya iliyotolewa Alhamis inaeleza kwamba ujumbe wa rais wa China Xi Jinping ulinunua maelfu ya kilo za pembe haramu za ndovu katika ziara yao mwaka 2013 nchini Tanzania.

Shtuma hizo zilitolewa katika ripoti ya taasisi inayofuatilia maswala ya Mazingira “Environmental Investigation Agency” kwamba mahitaji ya Wachina kwa pembe haramu za ndovu yanatishia idadi ya Tembo wa Tanzania.

Taasisi hiyo imesema ujumbe wa China uliitumia ziara ya Machi mwaka 2013 kutoa kwa magendo pembe za ndovu nje ya nchi kwa kutumia vifurushi vya kidiplomasia kwenye ndege ya rais Xi Jingping.

Ripoti ya taasisi hiyo yenye makao yake Uingereza, ilielezea wafanya biashara ya magendo ya pembe za ndovu jijini Dar es salaam na kusema kuwa ununuzi wa pembe hizo ulifanya bei yake kupanda maradufu.

Inasema kilo moja ya pembe za ndovu iligharimu dola za kimarekani 700. Pia inasema wanadiplomasia wa China, maafisa wa kijeshi, pamoja na wafanya biashara wa China siku za nyuma walitumia ziara kama hizo kununua shehena kubwa ya pembe za ndovu.

XS
SM
MD
LG