Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 19:18

Maafisa wanne wa MV Spice Islander washtakiwa kwa ajali ya meli


Jamaa wakiangalia kuwatambua ndugu zao ambao wamepoteza maisha katika ajali ya meli iliyotokea huko Zanzibar. Meli hiyo ilikuwa ikisafiri kwenda Pemba na ilipata ajali huko Nungwi. Jamaa hao walifika katika uwanja wa Maisara kuwatambua ndugu zao.
Jamaa wakiangalia kuwatambua ndugu zao ambao wamepoteza maisha katika ajali ya meli iliyotokea huko Zanzibar. Meli hiyo ilikuwa ikisafiri kwenda Pemba na ilipata ajali huko Nungwi. Jamaa hao walifika katika uwanja wa Maisara kuwatambua ndugu zao.

Mmiliki wa meli MV Spice Islander ni miongoni mwa washtakiwa

Waendesha mashtaka huko Zanzibar wamewashtaki watu wanne kuhusiana na uzembe unaohusiana na ajali ya meli iliyotokea Jumamosi iliyopita katika bahari ya hindi na kuua watu zaidi ya 200.

Meli hiyo MV Spice Islander, ilizama wakati ikifanya safari katika visiwa vitatu vya Zanzibar.

Waendesha mashtaka wamewashtaki nahodha wa meli, Abdallah Kinyayite, akiwa hayupo mahakamani kwasababu bado hajapatikana na haijulikani kama alinusurika katika ajali hiyo.

Watu wengine watatu wanaokabiliwa na mashtaka ni afisa wa boti hiyo, Abdallah Mohammed, mmiliki wa meli, Yusuf Suleiman Jussa na afisa wa Zanzibar anayehusika na ukaguzi wa abiria, Silima Nyango Silima.

Meli hiyo ilikuwa imebeba abiria wengi zaidi kuliko uwezo wake, ukiongezea na mizigo ambapo ndani ya meli pia kulikuwa na magari na vifaa vya ujenzi vya nyumba. Maafisa wanasema watu 600 waliokolewa.

Ijumaa zoezi la kutafuta miili ya wale waliopotea ambalo lilifanywa na waokozi, wakiwemo wazamiaji wa kikosi cha navy lilisitisha operesheni hiyo.

Idadi ya vifo mpaka hivi sasa inaelezewa ni watu 203 ndiyo waliopoteza maisha yao.

XS
SM
MD
LG