Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 22, 2025 Local time: 03:20

Maafisa Burkina Faso wanafanya uchunguzi kuhusu jaribio jipya la kuvuruga amani


Burkina Faso National political forum on the transition
Burkina Faso National political forum on the transition

Mwendesha mashtaka alisema katika taarifa Jumatano jioni kwamba "ushahidi wa kwanza" ulioanza kuchunguzwa baada ya kupatikana taarifa kutoka kwa mfichua siri  imedhidirisha kwamba "wanajeshi walikuwa wanajiandaa kuvuruga taasisi za serikali"

Maafisa wa ofisi ya muendesha mashtaka ya Burkina Faso wanasema wanafanya uchunguzi kutokana na jaribio jipya la "kuvuruga utulivu" wa taifa hilo, la Afrika magharibi, lililoongozwa na afisa mwandamizi anaeheshimiwa nchini humo

Mwendesha mashtaka alisema katika taarifa Jumatano jioni kwamba "ushahidi wa kwanza" ulioanza kuchunguzwa baada ya kupatikana taarifa kutoka kwa mfichua siri imedhidirisha kwamba "wanajeshi walikuwa wanajiandaa kuvuruga taasisi za serikali"

Moja kati ya nchi masikini zaidi duniani, Burkina Faso tayari imeshuhudia mapinduzi mawili yaliyofanywa na maafisa wa jeshi wasioridhika mwaka huu ambayo yameliweka jeshi madarakani.

Miongoni mwa waliopanga njama hizo ni afisa mkuu wa sita katika jeshi Charles Neboa na Sajent Adama Traore, kulingana na mfichua siri aliyenukuliwa katika taarifa hiyo.

"Walikuwa wakiwasiliana na kitengo cha 'green mamba' cha luteni kanali Emmanuel Zoungrana na walikusudia kufanya mashambulizi ya wakati mmoja kwenye redio na televisheni ya Burkina Faso (RTB), gereza la jeshi (Maca) ambapo afisa huyu alikuwa amezuiliwa kwa vitendo kama hivyo, na makazi ya mkuu wa nchi," nahodha Ibrahim Traore, mwendesha mashtaka alisema.

Zoungrana alikuwa amekamatwa Januari 14 akishukiwa "kujaribu kuyumbisha taasisi za serikali" na orodha ndefu ya mashtaka ikiwa ni pamoja na wizi, kughushi na utakatishaji fedha.

Wakati huo Burkina Faso iliongozwa na Rais Roch Marc Christian Kabore ambaye alikuwa ameshinda tena uchaguzi wa 2020.

XS
SM
MD
LG