Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 20:44

Lukashenko anasema nchi yake imeanza kuchukua silaha za nyuklia za Russia


Rais wa Belarus, Alexander Lukashenko

Upelekaji silaha huo Belarus ni hatua ya kwanza ya Moscow ya ubabe wa vita kama hivyo, silaha za nyuklia za masafa mafupi ambazo zinaweza kutumika kwenye uwanja wa vita, nje ya Russia tangu kuanguka kwa Umoja wa Sovieti

Rais wa Belarus Alexander Lukashenko amesema nchi yake imeanza kuchukua silaha za nyuklia za Russia ambazo baadhi yake alisema zina nguvu mara tatu zaidi ya mabomu ya atomiki ambayo Marekani ilidondosha huko Hiroshima na Nagasaki mwaka 1945.

Upelekaji silaha huo ni hatua ya kwanza ya Moscow ya ubabe wa vita kama hivyo, silaha za nyuklia za masafa mafupi ambazo zinaweza kutumika kwenye uwanja wa vita, nje ya Russia tangu kuanguka kwa Umoja wa Sovieti.

Tuna makombora na mabomu ambayo tumeyapokea kutoka Russia, Lukashenko alisema katika mahojiano na kituo cha televisheni cha taifa, cha Rossiya-1, ambayo yaliwekwa kwenye kituo cha habari cha serikali cha Belta, katika Telegram Channel ya Belarus.

Rais wa Russia, Vladimir Putin alisema siku ya Ijumaa kwamba Russia, ambayo itabaki na udhibiti wa silaha za nyuklia, itaanza kuzipeleka nchini Belarus baada ya vifaa maalum vya kuhifadhia silaha hizo kuwekwa tayari.

Kiongozi huyo wa Russia alitangaza mwezi Machi kuwa amekubali kupeleka silaha za nyuklia nchini Belarus, akielezea Marekani inapeleka silaha hizo katika nchi kadhaa za Ulaya kwa miongo kadhaa.

Forum

XS
SM
MD
LG