Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 07:58

Lipumba ajiuzulu uenyekiti wa CUF


Profesa Ibrahim Lipumba kiongozi wa chama cha upinzani CUF Tanzania
Profesa Ibrahim Lipumba kiongozi wa chama cha upinzani CUF Tanzania

Siasa za upinzani kuelekea uchaguzi mkuu nchini Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu zinazidi kutoa sura mpya. Mshikamano ndani ya umoja wa katiba ya wananchi UKAWA waliotangaza kusimamisha mgombea mmoja wa urais na kuachiana majimbo unaelekea kuzorota zaidi kutokana na tofauti zinazojitokeza siku hadi siku.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:54 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Pigo jingine kubwa ndani ya UKAWA lilitokea Alhamis baada ya kumsimamisha Bwana Edward Lowassa kama mgombea wake wa urais na Juma Duni Haji kama mgombea mwenza, sasa mwenyekiti mwenza wa umoja huo na mwenyekiti wa taifa wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba ametangaza kujiuzulu wadhifa wake ndani ya chama hicho cha CUF.

Prefesa Ibrahim Lipumba
Prefesa Ibrahim LipumbaBwana Lipumba alitoa uamuzi huo mapema Alhamis baada ya kuzuka sintofahamu ya hatima yake ndani ya CUF katika siku kadhaa zilizopita.

Akiwa amefuatana na watu wawili ambao hawakutambulika mara moja Profesa Lipumba alifika katika hotel ya Peacock ya jijini Dar Es Salaam akiwa ameshika mkoba uliokuwa na katiba iliyopo sasa na katiba inayopendekezwa kisha alianza kutoa historia ya kujiunga kwake na harakati za kukiongoza chama hicho mpaka hivi sasa na kueleza kuwa dhamira yake ndiyo inamsuta kutokana na kile alichodai kuwa viongozi walioingizwa katika UKAWA kwa sasa ndio walewale waliokuwa wanapinga katiba Pendekezwa iliyoandaliwa na jaji Warioba.

Profesa Lipumba akihutubia wanachama wa CUF
Profesa Lipumba akihutubia wanachama wa CUF

​Hata hivyo Profesa Lipumba aliwaomba radhi wanachama wake na wananchi kwa uamuzi wake huo wa ghafla katika kipindi hiki ambacho walikuwa na matumaini ya mabadiliko

Profesa Lipumba alielezea hatma yake sasa baada ya kujiuzulu wakati huu kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Wakati huo huo katibu mkuu wa chama cha Maendeleo na Demokrasia-CHADEMA Wilbroad Slaa naye alitangazwa kupumzishwa ili kutafakari hatma yake baada ya madai kwamba hakuridhishwa na utaratibu wa kumpata mgombea wa urais ndani ya Umoja huo.

XS
SM
MD
LG