Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 22:12

#BALonVOA2021 : Ligi ya NBA inayojumuisha timu za Afrika kuanza Mei 16 KigaliNembo ya BAL ya sherehe za uzinduzi katika Uwanja wa Kigali, Kigali, Rwanda, Desemba 19, 2019.
Nembo ya BAL ya sherehe za uzinduzi katika Uwanja wa Kigali, Kigali, Rwanda, Desemba 19, 2019.

Kati ya Mei 16 na Mei 30, 2021, Ligi la Mpira wa Kikapu Afrika (BAL) itazileta pamoja timu za Kiafrika 12 mjini Kigali, mji mkuu wa Rwanda, mwaka mmoja baada ya tarehe iliyopangwa awali kupita, kutokana na virusi vya corona.

Michuano ya BAL ilikuwa awali imepangwa kufanyika Machi 13, 2020, kutoka Dakar, Senegal, lakini iliakhirishwa kwa sababu ya janga la virusi vya corona.

Mashindano haya yanatokana na ushirikiano kati ya NBA na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Kikapu.

Timu kutoka nchi 12 za Afrika zitashiriki huko Algeria, Angola, Cameroon, Misri, Madagascar, Mali, Morocco, Msumbiji, Nigeria, Rwanda, Senegal na Tunisia.

Hii ni hatua ya kwanza ya NBA kuanzisha ligi nje ya Amerika Kaskazini.

Kundi A

1. US Monastir (Tunisia) ikiwa na mchezaji nyota Ater Majok

2. Rivers Hoopers (Nigeria) ikiwa na mchezaji nyota Ben Uzoh

3. Patriots (Rwanda) ikiwa na mchezaji nyota Aristide Mugabe

4. GNBC (Madagascar) ikiwa na mchezaji nyota Cameron Ridley

Kundi B

  1. Petro de Luanda (Angola ) ikiwa na mchezaji nyota Aboubakar Gakou
  2. AS Salé (Morocco) ikiwa na mchezaji nyota Eric Kibi.
  3. AS Police (Mali) ikiwa na mchezaji nyota Badra Samake.
  4. FAP (Cameroon) ikiwa na mchezaji nyota Ebaku Akumenzoh.

Kundi C

  1. Zamalek (Egypt) ikiwa na mchezaji nyota Anas Osama Mahmoud.
  2. AS Douanes (Senegal) ikiwa na mchezaji nyota Chris Cockley.
  3. GS Pétroliers (Algeria) ikiwa na mchezaji nyota Mohamed Seddik Touati.
  4. Ferroviário de Maputo (Msumbiji) ikiwa na mchezaji nyota Alvaro Calvo Masa

XS
SM
MD
LG