Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, sheria hiyo iliyopitishwa mwaka jana inadai “kulinda hadhi pamoja na tabia za umma,” bila kufafanua kwa kina.
HRW lenye makao yake mjini New York kupitia taarifa limesema kwamba “ Ni lazima baraza la wawakilishi la Libya litathmini upya sheria ya 2022 ya kupinga uhalifu wa kimitandao, inayominya uhuru wa mazungumzo.
Libya ilitumbukia kwenye ghasia 2011 baada ya kuondolewa kwa dikteta Moamer Kadhafi, na imegawanyika kati ya serikali mbili, moja ikiwa magharibi kwenye mji mkuu wa Tripoli, na nyingine mashariki mwa nchi ikiongozwa na Khalifa Haftar pamoja na baraza la wawakilishi.