Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 01:18

Liberia yaruhusu uraia pacha


Rais wa Liberia George Weah
Rais wa Liberia George Weah

Liberia imeruhusu uraia pacha, na hivo kubatilisha marufuku ya muda mrefu iliyochukuliwa na baadhi ya watu kama ya kinafiki kwani wasomi wengi walikuwa na uraia wa Marekani kwa siri.

Mswada huo ambao ulisainiwa kuwa sheria na Rais George Weah siku ya Ijumaa na kuthibitishwa na shirika la habari la AFP Jumapili, ulipitishwa na Bunge na baraza la Seneti siku ya Jumanne.

Inarekebisha sheria ya utaifa wa nchi hiyo ya Afrika magharibi, kuruhusu Waliberia kusalia raia baada ya kupata uraia wa pili.

Liberia, nchi iliyoanzishwa na Wamarekani, ina idadi kubwa ya raia waishio nchini hapa Marekani. Takriban watu 100,000 walioazaliwa nchini Liberia waliishi Marekani kati ya mwaka wa 2008 na 2012, kwa mujibu wa takwimu za sensa ya Marekani.

Raia wenye urai pacha hata hivyo, hawataruhusiwa kuhudumu kama rais, waziri wa fedha na mkuu wa benki kuu au kushikilia nyadhifa muhimu katika vyombo vya usalama wa taifa na sheria.

“Iwapo mtu kama huyo anataka kugombea kwenye uchaguzi, lazima aache kabisa uraia wa nchi nyingine angalau mwaka mmoja kabla ya kuwasilisha maombi kwa tume ya taifa ya uchaguzi, unaeleza mswada huo.

XS
SM
MD
LG