Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 09, 2024 Local time: 13:10

Lesotho yatangaza kufanya uchaguzi mkuu


waziri mkuu wa Lesotho Thomas Thabane katika picha
waziri mkuu wa Lesotho Thomas Thabane katika picha

Uchaguzi mkuu nchini Lesotho utafanyika mwishoni mwa mwezi februari miaka miwili mapema kuliko ilivyopangwa. Tangazo la Alhamisi limekuja baada ya viongozi wa serikali ya ushirika kutia saini makubaliano yenye lengo la kutekeleza maamuzi ya kupata amani ya kudumu katika nchi hiyo ya kifalme.

Naibu rais wa afrika kusini Cyril Ramaphosa alitajwa kuwa mpatanishi wa Lesotho mwezi uliopita wakati SADC inajitahidi kupata suluhu ya changamoto za kisiasa kufuatia jaribio la mapinduzi Augusti 30.

Waziri mkuu Tom Thabane aliangalia kwa upweke wakati Ramaphosa alipotangaza kwamba bunge nchini humo litaanza tena vikao octoba 17.

Vikao vya bunge vitakuwa ni kupitisha bajeti na kujadili masuala yote yanayohusu kuitisha uchaguzi wa mapema. Uchaguzi mkuu utafanyika mwishoni mwa mwezi februari mwaka 2015 na tarehe ambayo itachaguliwa na mfalme. Bunge ambalo litakutana tena, litavunjwa mwanzoni mwa desemba mwaka 2014 ili kuiandaa nchi kwa uchaguzi mkuu.

Bwana Thabane ataongoza serikali ya mseto – ya kwanza ya aina yake katika historia ya nchi hiyo, lakini hii ni kama ile iliyokuwa na matokeo ya uharaka wa kisiasa mwaka 2012 wakati uchaguzi uliposhindwa kumpata mshindi .

Jaribio la kukamata madaraka mwezi Augusti lilliongozwa na kamanda wa jeshi la ulinzi la Lesotho tlali kamoli aliyekataa kujiuzulu licha ya kufukuzwa kazi na rais na ameshutumiwa kwa kupanga mashambulizi dhidi ya polisi na wapinzani wa kisiasa.

XS
SM
MD
LG