Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 20:24

Mawakili wakubali rufaa ya Lema isimamishwe


Bendera ya cha upinzani cha Chadema nchini Tanzania.
Bendera ya cha upinzani cha Chadema nchini Tanzania.

Sisi kama mawakili tunaliangalia suala la dhamana ya Lema kwa macho ya kisheria, na kwa hamu kubwa tunasubiri kesi ya msingi, amesema wakili wa Lema, Peter Kibatala.

Mawakili wa Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chadema, Godbless Lema wamekubali rufaa ya serikali kuanza kusikilizwa kwa njia ya maandishi.

“Tumeona kwa kuwa matokeo ya rufaa ni moja, rufaa ya Lema isimamishwe mpaka pale rufaa ya serikali itapowasilishwa kesho katika mahakama kuu,” alisema wakili wa Lema, Peter Kibatala.

Aliongeza Lema amerejeshwa rumande akisubiri masuala haya ya kisheria yakamilike.

Aliongeza kusema kuwa siku ya Ijumaa mawakili wa Lema watawasilisha hoja zao kupinga uamuzi wa mahakama ya hakimu mkazi kumnyima mteja wao dhamana.

Lakini alisema kuwa Jaji wa Mahakama Kuu alitoa nafasi kwa pande zote mbili kuwasilisha hoja za ziada, na kuwa wao wataendelea kusimama pale pale kwamba wanapinga uamuzi wa mahakama hiyo ya chini kumnyima mteja wao dhamana.

Wakili huyo alisema kuwa Januari 2 upande wa serikali utakuwa na nafasi ya kujibu hoja na uamuzi utatolewa na mahakama kuu Januari 4.

Mnamo Novemba 11, Hakimu Mkazi alimpa Lema dhamana lakini kabla ya kutoa masharti ya dhamana hiyo upande wa serikali ulitoa notisi ya kukata rufaa.

“Lema alipata dhamana lakini kabla masharti hayajatolewa na hakimu upande wa serikali wakatamka wanakusudia kukata rufaa,” alisema wakili wake.

“Sisi kama mawakili tunaliangalia suala la dhamana ya Lema kwa macho ya kisheria, na kwa hamu kubwa tunaisubiri kesi ya msingi,” alisema.

Alipoulizwa kuhusu hali ya Lema, Wakili wake alisema kuwa iko imara na anaamini kwa asilimia 100 katika kile anachokiamini; mapambano ya uhuru wa kuzungumza.

Lema anashtakiwa kwa kutumia lugha ya uchochezi inayoweza kusababisha hali ya sintofahamu.

XS
SM
MD
LG