Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 19:41

LeBron James aamua kurudi Cleveland


Cleveland Cavaliers Awaits LeBron James' Return
Cleveland Cavaliers Awaits LeBron James' Return

Mchezaji nyota wa mchezo wa basketball hapa Marekani LeBron James ametangaza kuwa ataondoka timu ya Miami Heat na kurudi timu yake ya zamani Cleveland Cavaliers.

Uamuzi huo wa LeBron James ulikuwa unasubiriwa kwa hamu baada ya Miami Heat kushindwa katika fainali ya ligi na San Antonio Spurs mwanzoni mwa mwezi Juni. LeBron James alishinda ubingwa wa NBA mara tatu na timu ya Miami Heat.

Kabla ya kwenda Miami Heat LeBron James aliichezea Cleveland Cavaliers timu ambayo ilimchukua toka shule ya sekondari, na kuondoka kwake katika timu hiyo miaka minne iliyopita kuliwakasirisha sana wakazi wa Cleveland.

XS
SM
MD
LG