Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:36

Lagarde wa Ufaransa, Mkuu mpya wa IMF


Christine Lagarde mkuu mpya wa shirika la IMF
Christine Lagarde mkuu mpya wa shirika la IMF

Ataanza muhula wake wa miaka mitano Julai 5 na anakuwa mwanamke wa kwanza kuongoza shirika hilo la fedha duniani

Shirika la Fedha la Kimataifa - IMF - limepata kiongozi mpya. Ni Christine Lagarde ambaye mpaka uteuzi wake huu mpya alikuwa Waziri wa Fedha wa Ufaransa.

Bodi ya Utendaji ya IMF ilitangaza mjini Washington Jumanne mchana kuwa imemchagua Lagarde kuongoza shirika hilo la kimataifa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia Julai 5, 2011. Bi Lagarde anachukua nafasi ya Dominique Strauss-Kahn, pia raia wa Ufaransa, ambaye alilazimika kujiuzulu baada ya kutiwa nguvuni kwa madai ya kubaka mwanamke mmoja mfanyakazi wa hoteli mjini New York mwezi uliopita. Alikanusha mashitaka alipotokea mahakamani mjini New York.

Lagarde mwenye umri wa miaka 55 atakuwa mwanamke wa kwanza kuongoza taasisi hiyo tangu ianzishwe mwaka 1944. Kabla ya kuwa waziri wa fedha wa Ufaransa alikuwa waziri wa biashara za nje wa nchi hiyo kwa miaka miwili. Bi Lagarde ana uzoefu wa miaka mingi kama mwanasheria katika maswala ya biashara na kazi.

XS
SM
MD
LG