Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 09, 2024 Local time: 13:21

Joto laongezeka kwenye ziwa Tanganyika


Tanzania
Tanzania

Wanasayansi wanasema hali ya joto imezidi kwenye ziwa Tanganyika kuliko wakati wowote ule katika kipindi cha miaka 1,500 iliyopita.

Wanasayansi wanasema ziwa Tanganyika limezidi joto kuliko wakati wowote ule katika kipindi cha miaka 1,500 iliyopita na kutishia wanyama pori na mamilioni ya watu wanaolitegemea maji ya kunywa na samaki.

Uchunguzi mpya uliotangazwa jana na jarida la Nature Geoscience unalaumu shughuli za binadamu kwa kuongezeka kwa joto la ziwa hilo.

Waandishi wa ripoti hiyo wanasema, matokeo ni kwamba maji ya juu ya ziwa hilo yenye joto hayachanganyiki vizuri na maji yalio baridi zaidi chini ya ziwa hilo. Wanasema hali hiyo inatishia akiba ya chakula kwa samaki, kwa sababu maisha ya mimea iliyo karibu na maeneo ya juu haipati virutubisho muhimu kutoka chini ya ziwa.

Ziwa Tanganyiuka ni la pili duniani lenye kina kirefu ambalo watu milioni 10 wanategemea kupata maji na samaki.

XS
SM
MD
LG