Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 29, 2023 Local time: 22:09

Kuwait yaishauri Qatar kuvumilia baada ya kutengwa kidiplomasia


Wasafiri walioathiriwa na vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Qatar wakiwa uwanja wa ndege wa Hamad International Airport (HIA), Doha.

Waziri wa mambo ya nje wa Qatar amesema Jumanne kuwa Kuwait imemtaka emir wa Qatar kuahirisha hotuba yake na kutoa muda zaidi kuwezesha suluhu kupatikana.

Kauli imekuja kufuatia mgogoro ulioibuka wakati Saudi Arabia, Misri, Bahrain na Falme za Kiarabu (UAE), Yemen na Maldives walipositisha mahusiano ya kidiplomasia na Qatar.

Kumekuwa na mtiririko wa matangazo yakiituhumu Qatar kuwa inasaidia ugaidi, kitu ambacho imekanusha.

Sheikh Mohammed Bin Abdulrahman Al Thani amesema katika mahojiano na kituo cha habari cha Al Jazeera kuwa Kuwait ilikuwa makini katika kutatua mgogoro kama huu miaka mitatu iliyopita na wanajumuia wengine wa nchi sita za Baraza la Ushirikiano wa Ghuba la Uajemi.

Shirika la taifa la habari la Kuwait KUNA limesema Emir wa nchi hiyo, Sheikh Sabah al-Ahmad al-Sabah, amemshauri mtawala wa Qatar emir, Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, “kufanya uvumilivu na kujizuilia kuchukua hatua ambazo zitaongeza mvutano katika hali hii ya sasa.”

Sheikh Mohammed ameiambia Al Jazeera nchi yake “ilikuwa haina fununu yoyote kuwa mgogoro huu ulikuwa uko njiani kutokea” na kuwa masuala haya yangeliweza kuzungumziwa katika mkutano wa GCC au katika mkutano wa Arab-Islamic American Summit mwezi uliopita.

Nchi hizo zilizoiwekea vikwazo Qatar zimesema kuwa zimeondowa maafisa wake wa kidiplomasia kutoka katika nchi yenye utajiri wa gesi na kusitisha safari za anga na baharini kwenda Qatar. Kadhalika shirika la ndege la Qatar limetangaza kusitisha safari zake za ndege kwenda Saudi Arabia.

Misri imempa balozi wa Qatari masaa 48 kuondoka Cairo, wakati nchi za Ghuba ya Uajemi zimetoa kwa raia wa Qatari siku 14 kuondoka katika nchi zao.

Saudi Arabia, ambayo inaongoza umoja wa mataifa yanayopigana kuisaidia serikali ya Yemen, amesema pia vikosi vya Qatar vitaondoshwa kutoka katika mapambano hayo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG