Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 01, 2022 Local time: 11:20

Kutahiri huwenda ikazuia saratani ya kibofu cha mkojo


Mwanasayansi akifanya utafiti wa saratani katika maabara

Utafiti unaonyesha wanaume wanaotahiri wana nafasi ndogo kuugua saratani ya kibofu cha mkojo

Utafiti unaonyesha kuwa wanaume wanaotahiriwa mapema kabla ya tendo la kwanza la ngono wana uwezekano mdogo wa kuugua saratani hiyo ya kibofu cha mkojo. Utafiti huo unasema kuwa wanasayansi wanadhani kutahiri wanaume mapema kunapunguza uwezekano wa maambukizo yanayosababisha saratani hiyo.

Mtafiti mkuu Jonathan Wright wa chuo kikuu cha Washington katika jimbo la Seattle anasema alianza kufanya utafiti huo kubaini ikiwa kuna uhusiano kati ya tendo la kutahiri na saratani ya kibofu cha mkojo baada ya utafiti mwingine kuonyesha kuwa wanaume waliotahiriwa wana uwezekano mdogo wa kuambukizwa maradhi ya ukimwi ikilinganishwa na wenzao wasiotahiriwa.

Mtafiti Wright anadhania kuwa huenda tendo la kutahiri likazuia au kusaidia kutopata saratani ya kibofu cha mkojo. Na katika utafiti wake alilinganisha makundi mawili ya wanaume.Takriban wanaume 1,700 waliokuwa wakiugua saratani ya kibofu cha mkojo na wengine 1,700 wasiougua saratani hiyo.

Watafiti waliwauliza wote ni lini walitahiriwa na kisha kuchanganua matokeo yao. Aidha Wrights anaelezea kuwa uchunguzi huo unadhihirisha kuwa wanume waliotahiriwa wana uwezekano mdogo wa kuugua saratani ya kibofu cha mkojo, ingawa utafiti huo husemi kuwa kutahiri kunaondoa kabisa uwezekano wa mwanamume kuugua saratani hiyo. Kwa hiyo nini kinachoonyesha kuwa wanaume waliotahiriwa wana nafasi ndogo ya kuugua saratani ya kibofu cha mkojo? Wright anasema kuna mambo mawili.

Moja kuwa wasiotahiriwa wana ngozi inayoweza kuweka bakteria na kuchochea uwezekano wa kuugua. Ama labda wanaume wasiotahiriwa wana uwezekano mkubwa wa kuugua maradhi ya zinaa na hivyo kuongeza uwezekano wa kuugua saratani ya kibofu cha mkojo. Utafiti wake unaelezea utafiti mwingine uliobaini kuwa moja kati ya aina 6 za saratani kote duniani hutokana na maambukizo.

Utafiti wa Jonathan Wright kutoka chuo kikuu cha Washington-Seattle, juu ya uhusiano kati ya kutahiri na saratani ya kibofu cha mkojo umechapishwa katika jarida la Marekani la Saratani.

XS
SM
MD
LG