Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 22, 2024 Local time: 15:11

Kura zaendelea kuhesabiwa Sudan


Rais wa Sudan, Omar Hassan al-Bashir akipiga kura yake huko Khartoum, April 13, 2015.
Rais wa Sudan, Omar Hassan al-Bashir akipiga kura yake huko Khartoum, April 13, 2015.

Kura zinaendelea kuhesabiwa nchini Sudan baada ya siku nne za upigaji kura katika uchaguzi wa kitaifa ulioanza mwanzoni mwa wiki hii utaratibu uliokumbwa na utata wa kususiwa na chama kikuu cha upinzani nchini humo.

Huku matokeo ya uchaguzi huo yakiwa bado hayajatangazwa hadi baadae mwezi huu lakini yanatarajiwa kumpatia ushindi Rais Omar al-Bashir aliyepo madarakani hivi sasa na chama chake tawala cha National Congress Party.

Mkazi wa Khartoum katika upigaji kura wa April 13, 2015.
Mkazi wa Khartoum katika upigaji kura wa April 13, 2015.

Upigaji kura ambao awali ulikuwa wa siku tatu kuanzia Jumatatu hadi Jumatano uliongezewa muda wa siku moja zaidi hadi Alhamis ili kupata idadi ya watu walioshindwa kujitokeza katika siku za mwanzo.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi wa taifa, Mukhtar al-Assam alisema Rais Bashir anaonekana kushinda kura za kiti cha urais licha ya kwamba hatopata zaidi ya asilimia 50, mzunguko wa pili wa upigaji kura utafanyika.

Alisema matokeo kutoka kila kituo cha kupiga kura yatataangazwa haraka mara yanapopatikana lakini matokeo ya mwisho yatatolewa April 27.

Rais Bashir ambaye anatafutwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC juu ya mashtaka ya vita amekuwepo madarakani tangu mwaka 1989 na alishinda upigaji kura wa mwaka 2020 ambao upinzani ulishutumu ulijaa wizi.

Rais Omar al-Bashir wa Sudan
Rais Omar al-Bashir wa Sudan

Umoja wa ulaya, Marekani, Uingereza na Norway wote wameukosoa uchaguzi huo wakisema una mapungufu ya ahadi za mashauriano ya kitaifa ambayo yamesababisha nchi ya Sudan bila kuwa na utaratibu muafaka wa kisiasa.

Bwana Bashir ameahidi amani, maendeleo na kuimarisha uchumi wa nchi hiyo. Ni uchaguzi wa kwanza wa urais tangu Sudan Kusini ilipojitoa rasmi mwaka 2011 na kuwa taifa huru na kuchukua rasilimali nyingi za zamani za mafuta za Sudan.

XS
SM
MD
LG