Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 00:26

Kuondolewa rushwa na fursa kwa vijana kutamaliza Boko Haram - Kerry


U.S. Secretary of State John Kerry waves after a visit to the sultan's palace in Sokoto, Nigeria, Aug. 23, 2016.
U.S. Secretary of State John Kerry waves after a visit to the sultan's palace in Sokoto, Nigeria, Aug. 23, 2016.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry amesema kundi la Boko Haram la Nigeria litazuiwa tu endapo serekali itaweza kuondoa rushwa na kuwapatia vijana fursa.

Waziri Kerry ameyasema hayo nchini Nigeria, alipomtembelea kiongozi wa juu kiislamu Jumanne.

Ziara hiyo ya tatu na huenda ikawa ya mwisho kwake kama waziri wa mambo ya nje, imekuja wakati nchi hiyo ikikabiliwa na hali ya kudorora kwa uchumi na kuwepo kwa masuala kadhaa ya kuzorota kwa usalama.

Akiongea katika makazi ya Sultan wa Sokoto Saadu Abubakar, ambaye ni kiongozi wa juu wa Kislamu nchini Nigeria, Bwana Kerry amesema ni jukumu la serekali kuwapatia watu wake sababu ya kutojiunga na harakati za msimamo mkali.

XS
SM
MD
LG