Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 20, 2023 Local time: 17:52

Kundi lenye silaha huko Mali limejiondoa kuandaa rasimu ya katiba mpya


Ramani ya Mali ikionyesha pamoja nchi zilizo jirani

Katika taarifa iliyoonekana na shirika la habari la AFP siku ya Jumamosi, CMA ilielezea hilo pamoja na makundi mengine yote yenye silaha yaliotia saini makubaliano ya amani mwezi Desemba yalisitisha ushiriki katika mchakato wa amani kwa sababu ya "ukosefu wa nia ya kisiasa katika kuutetea"

Kundi lenye silaha nchini Mali ambalo lilitia saini makubaliano makubwa ya amani mwaka 2015 lilisema wiki hii linajiondoa katika juhudi za kuandaa rasimu ya katiba mpya.

Katiba mpya ni kiini cha mchakato wa amani na maridhiano uliopangwa kuirejesha nchi kutoka utawala wa kijeshi hadi wa kiraia ifikapo Machi 2024.

Vuguvugu la The Coordination of Azawad (CMA), muungano wa Tuareg ambao ulipigana na serikali kwa miaka mingi kabla ya kutia saini makubaliano ya amani huko Algiers mwaka 2015 uliulaumu utawala wa kijeshi.

Katika taarifa iliyoonekana na shirika la habari la AFP siku ya Jumamosi, CMA ilielezea hilo pamoja na makundi mengine yote yenye silaha yaliotia saini makubaliano ya amani mwezi Desemba yalisitisha ushiriki katika mchakato wa amani kwa sababu ya "ukosefu wa nia ya kisiasa katika kuutetea".

Uamuzi huo wa kwenda mbali zaidi na kususia kazi ya kuandika upya katiba umekuja saa chache baada ya Waziri wa Mambo ya Nje Abdoulaye Diop kuyashutumu makundi yenye silaha kwa "kukwamisha" juhudi za kuweka mchakato wa amani.

Kinyume chake, "kuzorota kwa wazi" kwa hatua za kuelekea amani kulitokana na "serikali kukataa bayana ili kulinda maslahi yao”, ilisema taarifa hiyo, ambayo ilitolewa Ijumaa.

CMA ilirudia ombi lake la kukutana na wapatanishi wa kimataifa kujadili uwezekano wa makubaliano ya amani, ambayo ilisema mwezi Desemba yalikaribia kuvunjika.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG