Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 04, 2024 Local time: 02:31

ISIS yaendeleza mauaji Libya


An image made available by propaganda Islamist media outlet allegedly shows members of the Islamic State parading in a street in Sirte, Libya.
An image made available by propaganda Islamist media outlet allegedly shows members of the Islamic State parading in a street in Sirte, Libya.

Wanamgambo wa kundi la Islamic State wamewaua karibu watu 49 ikijumuisha wapiganaji iliowashikilia, wapinzani wa kisiasa na wakazi wanaoshutumiwa kwa uchawi nchini Libya.

Mauaji hayo yamefanyika toka mwezi Febuari mwaka jana, katika mji wa bandari wa Sitre katika bahari ya Mediterranean, mji ambao ni ngome kuu ya kundi hilo nje ya Syria na Iraq wenye wapiganaji wengi, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na kundi la Kimataifa la Haki za Binadamu.

Wanamgambo wa Islamic State wamekuwa wakijiingiza katika vitendo vya utekaji, na kukamata dazeni ya wanamgambo wapiganaji wa Libya ambao mpaka sasa hawajulikani walipo mjini Sitre ambapo wengi wao wanahofiwa kuwawa kwa mujibu wa kundi la Human Rights Watch.

XS
SM
MD
LG