Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 06:40

Kundi la haki za binadamu lahofia kesi ya Kwoyelo


Thomas Kwoyelo, mkurugenzi mkuu wa zamani wa kundi la uasi la LRA
Thomas Kwoyelo, mkurugenzi mkuu wa zamani wa kundi la uasi la LRA

Mshkiwa Kwoyelo aliwekwa jela mwaka 2009 baada ya kupigana kwenye kundi la LRA, lililokua linapigana kaskazini ya Uganda

Kundi la kimataifa la kutetea haki za binadamu, linaeleza wasi wasi kuhusu kesi ya kwanza Uganda ya kiongozi mmoja wapo wa kundi la waasi la Lords Resistance Army. katika ripoti iliyotolewa leo human rights watch imesema matatizo ya kisheria na mipango ya utaratibu yanatishia kuhujumu kuweza kupatikana haki katika kesi ya Thomas Kwoyelo.

Mshkiwa Kwoyelo aliwekwa jela mwaka 2009 baada ya kupigana kwenye kundi la LRA, lililokua linapigana kaskazini ya Uganda. Wengi wa viongozi wake wanatafutwa na mahakama ya uhalifu ya kimataifa, ICC.

Lakini kesi ya kwoyelo inafanyika katika mahakama ya Uganda inayojulikana kama International Crimes Divisiona au ICD . Kesi hiyo ni ya kwanza kusikilizwa na ICD.

Elise Keppler wa kundi la human rights watch amesema ni muhimu kwa kesi nyingi kusikilizwa katika kiwango cha kitaifa kuliko mahakama ya uhalimu ya kimataifa.

Lakini katika kesi ya Kwoyelo kundi hilo la kimataifa linataja matatizo kadhaa. Mojawapo sheria ya msamaha ya Uganda ambayo imetumiwa kutoa samaha kwa baadhi ya wapiganaji wa LRA. Keppler amesema hakuna yeyote anayetakiwa kupewa msamaha kwa aina ya makosa ambayo kwoyelo anashutumiwa kuyafanya. Matatizo mengine katika kesi hiyo inaeleza ni ukosefu wa rasilimali za kutosha kwa utetezi, na ukosefu wa mipango ya kuwalinda mashahidi na kutokuwepo na habari kueleza raia juu ya kesi hiyo kwa wakazi wa kaskazini wa Uganda.

Human Rights Watch pia inasema ni muhimu kwamba mahakama inaruhusiwa kuwashitaki wanajeshi wa jeshi la Uganda baadhi yao wameshutumiwa kwa kufanya uhalifu mkubwa wakati wa ghasia kaskazini mwa Uganda.

Lakini wakili mwa mradi wa wakimbizi huko Uganda Stephen Okelo anasema litakua jambo zuri lakini haamini wanajeshi wanaweza kushtakiwa chini ya utawala huu wa sasa wa kampala.

XS
SM
MD
LG