Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 02:41

Nishati ya jua kusaidia wakulima Kenya


Teknologia ya kutumia upepo kunyunyuzia maji.
Teknologia ya kutumia upepo kunyunyuzia maji.

Kukuza nishati kutoka jua na upepo kwa kiwango kikubwa imekua na faida kubwa, lakini biashara hiyo inahitajimtaji mkubwa kufanikiwa.Hata hivyo hii leo mambo yamebadilika kujtokana na teknolojia mpya ambayo inamruhusu mtu kukuza nishati hiyo kwa bei nafu na kua na akiba ya kutosha.

Moja ya watu watakaofaidika Zaidi na teknolojia hiyo huko afrika ni wakulima kwani unyunyiziaji maji mashamabani huwenda ikawa shughuli yenye gharama ya juu kwa wakulima wadogo.

Wakati wa ukama ni lazima wanategemea mito, visima au hata kutumia mitambo ya mabomba yanayotumia diseli na huwenda yakawa ya gharama kubwa.

Mkulima Peter Mathenge kutoka Kenya anasema

"Tunatumia zaidi ya dola 300 kila mwezi kununua mafuta ya diseli."

Hali hiyo inaanza kubadilika kutokana na kwamba bei ya vioo vya kunasa miale ya jua zinashuka kila mara na hivyo wakulima hivi sasa wataweza kununua vifaa vya kunyunyiza maji kwa gharama nafu.

"Tukiwa na vifaa hivyo Agro Solar irrigation Kits tunatumia jua, na tunaitumia vizuri nishati hiyo. Mbali na hati hatuna haja tena kuandikisha wafanyakazi watatu kunyuweza maji wakati woteunapunguza hiyo gharama ambayo ni kupunguza kwa asili mia 30 matumiji ya ajira."

Mchana kutwa, pump inayotumia nishati ya jua inapeleka maji kwenye tangi lililo juu, huna haja ya kua na betri kuhovi nishati, kisha usiku unapoingia, mfereji unafunguka na maji yanaanza kunyunyizia shamba. Mathenge anasema teknologia hiyo imeongeza uzalishaji wake kwa maradufu.

Wakati huo huo nchini India, ambako thuluthi moja ya nyumba hazina nishati ya kutegemewa au hata umeme kabisa, wamiliki nyumba sasa wanaweza kununua mitambo midogo ya kunasa nishati kutokana na upepo anasema Arun Gerorge mkurugenzi wa kampuni ya Avant Garde innovation.

“Nishati yote watakayo zalisha kwa muda wote na chombo cha upepo ambayo inaweza kua ni miaka 20 basi itakua ni umeme wa bure kwao.”

Mtambo huo unaweza kuzalisha kati ya kilowatt 3 hadi 5 za umeme kwa siku, nishati ya kutosha kwa nyumba ya kawaida ya India.

Mtambo huo mpya utaweza kuwasaidia wahindi wengi zaidi kupata umeme hivi sasa.

XS
SM
MD
LG