Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 17, 2024 Local time: 18:56

Viungo vya binadamu kukuzwa kwenye mwili wa Nguruwe


Wanasayansi hapa Marekani wametangaza wiki hii kwamba wamepiga hatua kubwa katika juhudi zao za kujaribu kukuza viungo vya binadamu ndani ya mwili wa nguruwe.

Katika ripoti iliyochapishwa kwenye jarida la kisayansi la 'Panorama', wanasayansi hao wanatumia teknolojia mpya ya uhariri wa chembe chembe inayofahamika kama 'Gene Editing'.

Kwa miaka michache iliyopita, wanasayansi hao wamekuwa wakichunguza kwa makini jinsi vinasaba vinavyosaidia ukuaji wa kongosho yaani 'pancreas' kwa kiingereza, kwenye nguruwe, vianwea kusaidia kwa kiungu kama hicho, lakini cha binadamu.

Na sasa badala yake wanaweka chembe chembe za viungo vya binadamu kwa matarajio kuwa kongosho ya binadamu itakua.

Wataalamu katika chuo kikuu cha Davis, jimbo la California, wamesema kwamba wanaamini kuwa utafiti huo utasaidia kupunguza uhaba wa viungo vya binadamu.

Lakini teknolojia hiyo mpya imetajwa na wapinzani kama ambayo inakiuka maadili ya maumbile. Na kwa upande wa utaalamu, teknolojia hiyo pia inapingwa vikali na wanasayansi wengine kwa sababu ya maadili ya udaktari.

Wakosoaji wanasema kuwa endapo utafiti huo utafaulu na kutekelezwa kikamilifu, huenda ukaleta athari ambazo kwa sasa hazitarajiwi. Baadhi ya Wanasayansi wanadai kuwa huenda chembe chembe za binadamu zitakuwa na kufika kwenye ubongo wa nguruwe unaoendelea kukuwa.

XS
SM
MD
LG