Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 21, 2024 Local time: 19:28

Bobbi Kristina Brown afariki


Bobbi Kristina Brown, enzi za uhai wake
Bobbi Kristina Brown, enzi za uhai wake

Mtoto pekee wa mwimbaji maarufu marehemu Whitney Houston na mtalaka wake Bobby Brown, Bobbi Kristina Brown alifariki duniani Jumapili .

Bobbi Kristina Brown alifariki katika jengo la Peachtree Christian Hospice linalotoa huduma ya uangalizi maalumu wa kitabibu huko Duluth, Georgia ambako alipelekwa baada ya kuhamishwa kutoka hospitali moja huko Georgia kwa uangalizi zaidi wa kitabibu.

Binti huyo alikutwa ameanguka bafuni hapo Januari 31 na kisha kukimbizwa hospitali huku afya yake ikiripotiwa kuzorota mara kwa mara.

Bobbi Kristina Brown alizaliwa Machi 4, 1993 huko Livingston, New Jersey. Hadi mauti yalipomfika alikuwa na umri wa miaka 22.

XS
SM
MD
LG