Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 10, 2024 Local time: 04:11

Korea Kaskazini imekubali kushiriki Olimpiki - Korea Kusini


Maafisa wa ngazi za juu wa Korea Kaskazini na Korea Kusini wakutana.
Maafisa wa ngazi za juu wa Korea Kaskazini na Korea Kusini wakutana.

Afisa mmoja wa Korea kusini amesema Korea Kaskazini imesema iko tayari  kutuma ujumbe  wa ngazi ya juu kuhuduria mashindano ya Olympic ya msimu wa baridi mjini Pyeongchang.

Pendekezo hilo lilitolewa siku ya Jumanne wakati wa mkutano wa kwanza wa ana kwa ana katika kipindi cha miaka miwili kati ya nchi hizo mbili hasimu.

Naibu waziri wa ushirikaiano, Chun Hae Sung aliwaambia waandishi wa habari mjini Seoul kwamba Korea Kaskazini itatuma maafisa wa ngazi za juu, wanariadha na kikundi cha washangiliaji kwenye micheo hiyo itakayoanza Februari 9.

Aidha waziri huyo alisema Korea Kusini imependekaza mkutano mwingine wa kuziunganisha familia zilizotenganishwa na vita vya kati ya mwaka wa 1950 na 1953, ambavyo vilitenganisha nchi hizo mbili, ufanyike mwezi ujao.

XS
SM
MD
LG