Hatua hiyo imesababisha kutolewa kwa tahadhari ya dharura, na onyo la watu kuondoka katika sehemu za Korea Kusini na Japan.
Korea Kaskazini imesema itazindua seteleiti yake ya kijeshi ya kwanza kati ya Mei 31 na Juni 11 kuongeza uangalizi wa shughuli za Marekani.
Katika taarifa zilizotolewa na serekali za kimataifa, Korea Kaskazini imesema kuzinduliwa huko kutatumia roketi kwenda kusini, ambapo kutakuwa na hatua mbalimbali zitakazo zalisha mabaki na kudondoka katika Yellow Sea, na pia bahari ya Pacific.
Ving’ora vya tahadhari vilisikika katika mji mkuu wa Korea Kusini, Seoul majira ya saa 12 na dakika 32 asubuhi ya Jumatano, ikiwa ni tahadhari kwa wakazi kujiandaa kuondoka.
Baadaye taarifa ilitolewa ikieleza kuwa tahadhari hiyo ilifanyika kimakosa. Serekali ya Japan pia ilitoa tahadhari kama hiyo.
Forum